Monday, April 2, 2018

RAIS MSTAAFU KIKWETE AIOMBA SERIKALI KWA JICHO LA TATU, WEMA SEPETU ANG'ARA

Tags


RAIS Mstaafu, Jakaya Kikwete (JK),  amewapongeza wasanii wa filamu kwa jitihada zao na kuiomba Serikali kuwatazama kwa jicho la tatu ili kukuza tasnia hiyo.
Aliyasema hayo usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, katika tamasha la kimataifa la filamu la ‘Sinema Zetu’ lililoandaliwa na Azam Media.
JK alisema anaimani kwa hatua kubwa waliopiga wasanii hao inatokana na juhudi zao binafsi licha ya kukabiliwa na hali ngumu kifedha na kukosa elimu ya kutayarisha filamu.
“Wasanii wanajitahidi sana kwani ukiangalia wanafanya kazi katika mazingira magumu, kwa kutumia vifaa ambavyo sio bora na hata hao watayarishaji wa filamu hizi hawana elimu ya kutayarisha filamu.

“Watu wengi wanawalaumu kuwa hawatayarishi filamu bora, lakini tukumbuke kuwa hizi ni juhudi zao wenyewe, Azam mmeonesha njia na mmtekeleza wajibu wenu, serikali nayo ichukue sehemu yake” alisema Dk. Kikwete.
Aliongeza kuwa ikiwa sekta ya filamu itawezeshwa kikamilifu itachangia katika pato la taifa na kupunguza tatizo la ajira nchini kutokana na kuwa na uwezo wa kuajirio watu wengi kwa wakati mmoja.

Katika tuzo hizo Mlimbwende Wema Sepetu, aliibuka na tuzo mbili ikiwa ni pamoja naile ya mwigizaji bora wa kike pamoja na filamu bora ndefu kupitia filamu yake ya ‘The Heaven Sent’ baada ya kuwa shinda wapinzani wake akiwamo mwanadada Riama Ally.
Mbali na Wema msanii mwingine alitikisa katika tuzo hizo ni Salim Ahmed ‘Gabo’ aliyeshinda tuzo tatu ikiwamo ya mwigizaji bora wa kiume kupitia filamu yake ya ‘Safari ya Gwalu’
Chanzo: Bin Zubeiry