Raia 50 wa Ghana wafukuzwa Australia kwa kujifanya kuwa waandishi wa habari.

Zaidi ya raia wa Ghana 50 waliojaribu kuingia nchini Australia kinyemela wamekamatwa walipokuwa wakijaribu kuingia nchini humo kwa kujifanya kuwa waandishi wa habari
Raia hao walishikwa wakati waliposhindwa kujibu maswali kuhusu michezo.
Ingawapo walikuwa na nyalaka halali za kusafiria, walikamatwa na kushikiliwa baada ya kushindwa kujibu maswali rahisi kuhusu michezo.
Naibu Waziri wa Michezo wa Ghana,Pious Enam Hadidze, amesema kuwa wameanza uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Hata hivyo alisema wizara yake haikuwa na uhusiano yoyote na raia hao na haikuwahi kuwasaidia kupata visa hapo awali.
"Hatukuwa dhamini waandishi wa habari wowote, hatukuwadhamini wafuasi, hatukuwa dhamini mtu yeyote kwenda kaitka michezo ya jumuiya ya madola" aliiambia mtandao wa habari wa Graphic, nchini Ghana.
Posted by Lebabtv
Source: Bbc

MaoniMaoni Yako