Polisi Abakwa alipoenda Kumkamata Mbakaji


Askari Polisi mmoja wa kike huko Yorkshire Kusini, nchini England ameripoti kubakwa na mwanaume ambaye alikwenda kumkamata akiwa na askari mwingine kwa makosa ya jaribio la kubaka.

Mwanaume huyo alikuwa akihisiwa kufanya vitendo hivyo vya kujaribu kubaka watoto wa kike na ndipo askari huyo alipokwenda na mwenzie kumkamata ili afikishwe polisi.

Inaelezwa kuwa mwanamume huyo tayari amekwisha kamatwa na amefungulia mashtaka ya kujaribu kubaka, shambulio, unyanyasaji wa kijinsia na uharibifu wa makosa ya jinai


Source: udaku special
MaoniMaoni Yako