PICHA: Yanga walivofanya mazoezi leo

Na George Mganga
Licha ya kutotumika katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United Jumapili ya wiki iliyopita, wachezaji Donald Ngoma na Thaban Kamusoko wamefanya mazoezi leo.
Kamusoko na Ngoma wamekuwa miongoni mwa wachezaji wa Yanga waliojifua asubuhi ya leo Jamhuri Stadium mjini Morogoro, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha FC ya Ethiopia.
Wachezaji hao wahakucheza dhidi ya Singida kutokana na hali zao kiafya kuonekana bado hazijaimarika vizuri. 
Yanga imeweka kambi Morogoro kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa Jumamosi ya wiki hii Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Aprili 7 2018.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz