NUKUU USIZOZIJUA ZA WINNIE MANDELA  1. "Miaka niliyofungwa gerezani ilinifanya kuwa mkakamavu... Huwa sina tena hisia za woga ... Hakuna chochote ambacho naweza kukiogopa. Hakuna kitu ambacho sijatendewa na serikali. Hakuna uchungu ambao zijakumbana nao." Nukuu hii katika kitabu chake cha Lives of Courage: Women for a New South Africa(Maisha ya Ujasiri: Wanawake wa Afrika Kusini Mpya), inaashiria jinsi Bi Madikizela-Mandela alivyofanyiwa ukatili na serikali ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
  2. "Kwa viberiti vyetu na mikufu yetu tutaikomboa nchi hii." Tamko hilo, katika mkutano wa siasa mjini Johannesburg, aliashiria kwamba Bi Mandikizela-Mandela alikuwa ameidhinisha na kuunga mkono njia katili ya "kuweka mikufu" - njia ya kuweka matairi shingoni washukiwa wa usaliti na kuwachoma moto wakiwa hai
  3. Kuhusu kumpenda Nelson Mandela: "Nilikuwa na wakati mdogo sana kumpenda. Na upendo huo umedumu miaka hii yote ambayo tulitenganishwa... pengine kama ningepewa muda wa kutosha wa kumfahamu vyema zaidi pengine ningegundua kasoro nyingi, lakini nilikuwa tu na wakati wa kumpenda na kumkosa sana wakati wote."
  4. Kuhusu kusalia na jina la Mandela baada ya talaka: "Mimi ni mazao ya wananchi wa taifa hili. Mimi ni mazao ya adui wangu mkuu."
  5. Kuhusu wanawake: "Wengi wa wanawake huupokea mfumo dume bila kuuliza maswali na hata huutetea, kwa kuelekeza mahangaiko yao sio kwa wanaume bali dhidi yao wenyewe wakishindania wanaume walio wana wao wa kiume, wapenzi wao na waume zao. Kitamaduni, mke ambaye amedhalilishwa hujituliza na kuelekeza ghadhabu zake kwa wakwe. Kwa hivyo, wanaume huishia kuwatawala wanawake kupitia juhudi za wanawake wenyewe."
  6. Kuhusu serikali ya ANC: "Ninaamini kuna kitu ambacho ni kibaya sana katika historia ya taifa letu, na jinsi ambavyo tumeiharibu African National Congress."
Source: bbc
Na: Sabby@spoti.co.tz

MaoniMaoni Yako