Njombe Mji Wakubali Kilichotokea Wahamishia Majeshi Kwa Stand United Wenyewe Waahidi Kusalia Ligi Kuu Msimu Ujao. Soma Hapa Kusoma Zaidi.Mara baada ya kumalizika kwa mtanange wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Njombe mji na Simba sc klabu ya Njombe mji iemsema bado inayonafasi ya kuendelea kusalia kwenye ligi hiyo kwa msimu ujao kutokana na michezo iliyosalia.

Njombe mji kupitia kwa msemaji wake mkuu Hassan Macho imeeleza kuwa licha ya kupoteza mchezo wa leo bado vija wamepambana na Macho amewataka mashabiki kuendelea kuiunga mkono klabu hiyo kwenye michezo iliyosalia hususani mchezo dhidi Stand United ili kuhakikisha wanaondoka na alama tatu muhimu

Akizungumza na mwandishi wetu "Alexander Victor" , Macho amesema
"Timu yetu imecheza vizuri ispokuwa matokeo hayakuwa upande wetu!hivyo niwaombe wananjombe kwa umoja wetu tuwaunge mkono vijana kwa michezo iliyobakia."

Tunajua matokeo haya yanaumiza ila hatuna budi kusahau na kufikiria mchezo ujao dhidi ya Stand united utakachezwa ugenini tarehe 8.4.18.
Timu inatarajia kuondoka mjini Njombe tarehe 5.4.18. Kuelekea shinyanga kusaka point tatu muhimu.

Tumepoteza mchezo huu ila bado tunayo michezo mingine mbele yetu.
Kazi iliyopo mbele yetu ni ngumu tuombe mshikamano kuelekea michezo yetu ya lala salama kuinusuru timu yetu ili msimu ujao tuendelee kushuhudia ligi kuu hapahapa Njombe.
Mwisho niwashukuru benchi la ufundi chini ya kocha Ally Bushiri na wachezaji wote!kwa kuonyesha mabadiliko makubwa kwenye kikosi.
Tunaamini timu haitokuweza kushuka daraja. Hassan Macho Msemaji Njombe mji fc
MaoniMaoni Yako