Powered by Blogger.

Slider

Breaking

MICHEZO

HABARI

MAGAZETI

UDAKU

BURUDANI

VIDEOS

» »Unlabelled » Ni Ronaldo tena! Aiokoa Madrid kutoka kwa Juventus!


Ni kama ndoto, ama tuseme nikama bahati ya mtende! Amekuwa ni mchezaji muhimu kwa klabu yake, ameonesha umuhimu wake hasa pale anapohitajika! kwa lugha nyingine unaweza kabisa kumuita ni Mwokozi wa timu! Hakika huyu ndiye mchezaji bora kabisa! ni nani huyu? Wanamuita "a goal machine- the finisher himself " Christiano Ronaldo

Madrid walitakiwa kusubiria hadi dakika ya 98 ya mchezo wao dhidi ya Juventus kuwa na uhakika wa kusomga mbele katika hatua ya nusu fainali! Juventus walijipanga vizuri kuiadhibu Madrid nyumbani kwao, kwani waliweza kuta goli lao la kwanza katika dakika ya pili tu ya mchezo kupitia mshambuliaji wao Mario Mandzukic aliyekuwa mwiba mkali kwa safu ya ulinzi ya Madrid. Dakika ya 37 alikuwa Mandzukic tena aliyeipatia Juve, goli la pili.

Ikumbukwe kwamba Juventus walikuwa wanahitaji magoli manne kwa bila ili kuiondoa Madrid waliokuwa wana mtaji wa magoli matatu waliyojipatia nyumbani kwa Juventus.
Wakati Madrid wakiendelea kutoamini kinachotokea, Blaise Matuid alipeleka kilio cha tatu kwa Madrid baada ya kufunga goli safi kabisa katika dakika ya 61.

Ikiwa muda wa kawaida yaani dakika 90 zimeisha, refali aliongeza dakika 3 ambazo zilitosaha kabisa kwa Madrid kubadili muelekeo wa matokeo. Dakika ya 93 Madrid wakapata penati iliyotokana na Vazquez aliyepata pasi kutoka kwa Ronaldo kusukumwa na Benatia wa Juve.
Ronaldo aliipiga penati hiyo na kuipatia Madrid goli pekee lililowaokoa Madrid na kuwapeleka katika hatua ya nusu fainali.

Na: sabby@spoti.co.tz

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post