Ni nini hasa Walichonacho Mabinti Wa Kitanga? Tanga Kunani??


Imekuwa kawaida sana kusikia "ukienda Tanga haurudi leo"  mara " waja leo waondoka kesho" au "wja leo, kuondoka majaliwa" Hizi ni kauli ambazo ukizisikia wala hauhitaji kuuliza maana yake ni ninini au zinawahusu akina nani na wapi. Hii ni Tanga ninayoizungumzia, Kunani pale? Katika ulimwengu wa Mapenzi hapa Tanzania, tunaambiwa Tanga ndiko yalikozaliwa, hata Mwana FA na Kassim waliimba. Swali langu ni hili: Kunani Tanga? 

Kimsingi siyo suala la mazingira ya Tanga linalozungumziwa, ni suala la Mapenzi , yaani wanawake wa Tanga. Hawa ndiyo wanaaminika wakikushikilia mwanaume, katuuuu hautoki! utasahau hata jina la ulikotoka.. Wapo walioenda na mitaji yao kwaajili ya kufanya biashara kama ya Machungwa pale Muheza, au Mananasi na hata Nazi. Wengi wao wamebaki walowezi wa Tanga baada ya kushindwa kabisa kurejea kule walikotoka, kisa? Mabinti wa Kitanga! Ninajiuliza , Wanawake wa Tanga wana nini cha mno hadi kugeuka kuwa vifutio vya kumbukumbu za wanaume hawa? Tanga kunani pale??
Je! Ni watoto wa kimanga? ni watoto wa kiarabu? ni lugha ya ulimi ya wanawake wa Tanga wanaooongea na kudhihirisha kwamba ulimi hauna mfupa? ni Viuono vyao laini? ni Shanga viunoni kama alivyoimba Bwana Misosi? Ni mapishi? Ni nini basi kikubwa kilichopo Tanga, ni nini haswa walichonacho mabinti wa Kitanga ambacho Mabinti na dada zetu wa huku bara hawajajaliwa? Tanga Kunani pale?

Tafadhali, nifahamisheni maana nina safari ya kwenda Tanga siku si nyingi!.
MaoniMaoni Yako