Powered by Blogger.

Slider

Breaking

KITAIFA

VideoBar

This content is not yet available over encrypted connections.

KIMATAIFA

MAGAZETI

UDAKU

BURUDANI

SPOTI TV

» » Nedy Music afunguka kufanya kazi na Alikiba, kusaini WCB


Msanii wa muziki Bongo, Nedy Music amefunguka kuhusu mipango yake ya kufanya kazi na Alikiba pamoja na kusaini katika label ya WCB.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘One and Only’ ameiambia The Playlist ya Times FM kuwa mipango ya kufanya ngoma na Alikiba ipo ila anahitahitaji watu wamjue kwanza na sio wafanye kwa sababu wanajuana.
“Unajua usifanye kitu kimazoea, usifanye kitu kwakuwa unajuana na mtu nilitamani watu wajue uwezo wangu, nikiwa na maana hata pale ninapoenda na kazi nataka afanye na mimi basi pawe na urahisi na si kinyonge atafanya kwa kuwa tunajuana, kwa hiyo ni wazo bado lipo na panapo majaliwa litatokea,” amesema.
Kuhusu kusaini katika label ya WCB amesema ikitokea nafasi hiyo atasaini kwa sababu ni biashara, pia amekanusha taaarifa za kuachana na label yake ya PKP mara baada ya wimbo wake mpya kutoka bila kuwa na logo ya label hiyo.
PKP ni label ambayo inamilikiwa na msanii Ommy Dimpoz ambaye July 06, 2017 alisaini kufanya kazi na label ya  RockStar4000 inayofanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment.
by richard@spoti.co.tz
chanzo-bongo 5

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post