Mzee Akilimali anena baada ya Yanga kufungwa, kawambia Simba hivi pia..


Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amekubali kupoteza jana katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya watani zao wa jadi Simba. Akilimali ambaye ni mwanachama mkongwe wa klabu hiyo, amesema amekubali matokeo huku akieleza bado milango ya ubingwa kwa Yanga ipo wazi.
 Mapema baada ya mtanange huo kumalizika, mzee huyo alieleza kujifungia ndani na hayuko tayari kuonekana mtaani hivi sasa na pengine hata msikitini hatoweza kwenda kutokana na aibu ya kichapo. Akilimali amesema anaiombea Simba kwa sasa iweze kupoteza walau mechi mbili zijazo na Yanga washinde ili waweze kuendelea kuutetea ubingwa wa ligi msimu huu.

Yanga imejiwekea mazingira magumu ya kulibeba taji la ligi kutokana na kupoteza mchezo wa jana, kitu ambacho kinawafanya Simba wazidi kujinasibu na rekodi yao ambapo mpaka sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja. 
Source: Saleh Jembe Na: Agape Patrick Email: agape@spoti.cotz
MaoniMaoni Yako