Mwandila Ngoma hatocheza msimu huu Ngoma Alikuwepo katika Kikomo Cha Yanga SC Kilichokuwa kinajiandaa na Mchezo wa Ligi Kuu Bara Dhidi ya Simba SC lakini hakucheza baada ya Kupata Majeraha Mengine Mazoezini. Kocha Msaidizi wa Yanga SC Noel Mwandila Amesema kuwa Mshambuliaji Wao raia wa Zimbabwe Donald Ngoma hatocheza tena Msimu huu baada ya Majeraha yake kuwa Sugu, Mwandila Amesema kuwa Majeraha hayo yanahitaji muda zaidi kuweza kupona kabisa na Kurejea Uwanjani. Hata hivyo TETESI zinasema kuwa Yanga SC Itaachana na Mshambuliaji huyo Mara tu Ifikapo Mwisho wa Msimu huu kwa Kuwa Majeraha yake hayaponi. "Tumemvumilia Sana Ngoma Msimu huu lakini Majeraha yake hayaponi,hivi Sasa anahitaji muda mrefu kuweza kupona nadhani tumsubiri Msimu Ujao" Alisema Kocha huyo raia wa Zambia Ambaye Alikuwa Msaidizi wa George Lwandamina Kabla ya kutimkia ZESCO United pia kabakia Yanga SC kama Msaidizi wa Kocha Mpya Mwinyi Zahera.
Na: Agape Patrick Email: agape@spoti.cotz
Source: Soka Place 
MaoniMaoni Yako