Muigizaji wa sinema za Bollywood Salman Khan,ahukumiwa miaka mitano jela

Mahakama moja ya India imemhukumu nyota muigizaji wa sinema za Bollywood Salman Khan, hukumu ya miaka mitano jela kwa kuua aina mojawapo ya swala ambao ni adimu kupatikana duniani mwaka 1988.
Mahakama hiyo iliyoko Jodhpur imemtoza faini ya rupia 10,000 ($154; £109) kwa kosa hilo.
Amepelekwa korokoroni na anatarajiwa kusalia huko kwa muda.
Khan aliwaua swala wawili kwa jina blackbucks, ambao hulindwa na kuhifadhiwa, Magharibi mwa jimbo la Rajasthan alipokuwa akiigiza filamu.
Waigizaji wengine wanne walioshiriki naye uigizaji kwenye filamu hiyo, waliokuwa wamehukumiwa kwa kosa hilo na mahakama ya awali, walisamehewa.
Khan, 52 , anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama ya juu.
Wanahabari wamesema atasalia korokoroni kwa siku kadha.
Nini chanzo cha kesi ya Khan?
Hii ni kesi ya nne iliyowasilishwa dhidi ya mwigizaji huyo inayohusiana na uwindaji haramu wa wanyama wakati walipokuwa wakiigiza filamu ya Hum Saath Hain mwaka 1988.
Source: bbc
Na: sabby@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako