Mtibwa waongea kuhusu mechi yao vs simbs

Na George Mganga
Uongozi wa Mtibwa Sugar umesema hauna hofu na vinara wa Ligi Kuu Bara msimu huu, klabu ya Simba, kuelekea mchezo wa ligi Jumatatu ijayo.
Kupitia Msemaji wa timu hiyo, Thobias Kifaru, amesema wao wanajipanga kwa ajili ya kupigania alama tatu muhimu hivyo hana wasiwasi kuelekea mchezo huo.
Kifaru ameeleza kuwa wanaendelea na maandalizi yao hivi sasa na wapo tayari kwa mechi dhidi ya Simba itakayopigwa Jamhuri Stadium Jumatatu ya Aprili 9 2018.
Mtibwa itakuwa inaikairibisha Simba ikiwa nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi huku ikiwa imejikusanyia jumla ya alama 27.
Wakati huo Simba ambao wanapigania ubingwa wako nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 49 wakifuatiwa na watani wao wa jadi Yanga walio na 46.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako