Mpenzi Wangu Ananitafuna Kila Tulalapo: Msaada Tafadhali


Wana SPOTI.TZ Ninakuja kwenu siku ya leo kujaribu kutafuta msaada wa mawazo kutoka kwenu, huenda kuna mwingine anaehitaji msaada kama wangu ila kashindwa kufunguka. Ndugu zangu nipo katika mahusiano ya kimapenzi na mchumba wangu kwa mwaka mmoja sasa na hakika mipango yangu ni kumuoa mapema mwaka huu, yaani kabla hatujamaliza huu mwaka. 

Ila sasa tatizo limeibuka hivi karibuni, mpenzi wangu amegeuka kuwa VAMPIRE. Yaani kila tukikutana kunako sita kwa sita basi, ujue mwisho wa purukushani zetu ni lazima niende kuchoma sindano za tetenasi maana meno yooote 32, huwa yanaufanyia kazi mwili wangu hasa shingoni. Ninatafunwa kama simba afanyavyo akimkata swala, shingo yoote inakuwa na majeraha ya kung'atwa, nikimuuliza ananiambia " hizo ni love bite"  Sasa nitavumilia mpaka lini? na anaonekana anafurahia kweli hizo Love bite zake! 

Kwakweli ninahitaji msaada kwenye tuta, angalau mnishauri nifanyaje, nimuache? mwenyewe nampenda lakini ingawa na uhai wangu naupenda vilevile! maana tunakoelekea naona kabisaa hii shingo ataigeuza kitoweo chake! Ama mnadhani mnamfahamu Saikolojist angalau akamshauri? 

KUTOKA KWA MSOMAJI WETU


MaoniMaoni Yako