Mbunge Asema Diamond ni Nembo Ya Taifa, hivyo Serikali ifanye Haya yafuatayo:

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuwatumia wasanii hasa Diamond katika kuitangaza nchini.


Ngeleja ameyasema hayo jana Bungeni wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

“Bongo Flava imetutoa, tunamzungumzia msanii kama Diamond, tunaungana na Watanzania wote kumpongeza kwa hatua aliyofikia ya kutambuliwa kwamba awe miongoni mwa watu waliotunga wimbo maalum kwa ajili ya Kombe la Dunia mwaka huu,” amesema.

“Naamini huko atapoenda kutuwakilisha, naamini Wizara ya Maliasili itam-package kwenda kuitangaza nchi yetu Diamond kwa sababu yeye ni nembo ya Taifa, kwa hiyo ni muhimu kuwa na watu kama hawa katika taifa letu,” amesisitiza.

Diamond kwa kushirikiana na msanii kutoka Marekani, Jason Derulo wameimba wimbo unaokwenda kwa jina la Colours ambao ni maalum kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 inayotarajiwa kuanza June nchini Urusi. 

Source:udaku special
MaoniMaoni Yako