Mashabiki Yanga wacharuka wataka Nsajigwa atokeBaada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara jana, baadhi ya mashabiki wa Yanga wamemtaka Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa kuachia ngazi. Mapema baada ya mchezo kumalizika, mashabiki hao walianza kutupia lawama kwa Nsanjigwa, wakidai kuwa hana mbinu za kuendelea kuisaidia timu hiyo ipate matokeo, na badala yake ameisabishia kupoteza mchezo. Kwa mujibu wa Spots Xtra ya Clouds FM, mashabiki hao waliokuwa wamepandisha hasira kutokana na kufungwa na watani zao wa jadi Simba, wameuomba uongozi wa Yanga kuachana na Nsanjigwa wakieleza kuwa hana ujuzi wa kuendelea kuinoa Yanga. Yanga ilikubali kufungwa bao moja na Simba katika mchezo huo uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, bao hilo likitiwa kimiani na Erasto Nyoni kwenye dakika ya 37.

Na: agape Patrick Email: agape@spoti.co.tz

Source: Saleh Jembe
MaoniMaoni Yako