Manara awakutanisha alikiba na diamond


Na George Mganga
Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amewakutanisha wasanii wakubwa wanaotamba zaidi Tanzania na Barani Afrika kwa miaka ya hivi karibuni, Diamond Platnumz na Ali Kiba.
Haji Manara amewakutanisha wasanii hao kwa kuweka video zao pamoja katika akunti yake ya Instagram huku akiwaongelea kila mmoja kwa namna yake anayotambua vipaji vyao.
Manara amemuelezea Msanii Platnumz kuwa anajituma kwa kupambana zaidi huku akimfananisha na nyota wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo kuwa wote hupambana ili kupata kile wanachokihitaji.
Aidha, Manara amemzungumzia Kiba kama Msanii mwenye kipaji asilia kutokana na ukali wa toni ya sauti yake namna ilivyo huku akimfananisha na nyota wa FC. Barcelona Lionel Messi ambaye amekuwa hatumii nguvu nyingi mazoezini.
Imekuwa ni kawaida kwa Haji Manara kuwaongelea mara nyingi Platnumz na Kiba kwa kusema kuwa ni wasanii wakubwa ambao anatamani siku moja wakija kutoa wimbo pamoja.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako