Madrid Wasiombe kukutana na Liverpool ya Salah


London, England. Nyota wa zamani wa Liverpool, Newcastle na Manchester City, Craig Bellamy anaamini kwamba Real Madrid haiwezi kuimalizi kirahisi Liverpool kama wakikutana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Liverpool imeonyesha shoo ya maana wiki hii kwa kuimaliza Roma kwa mabao 5-2 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku Real Madrid nayo ikionyesha ukali wake kwa kuikamua Bayern Munich mabao 2-1 katika mechi nyingine ya kwanza ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini Bellamy anasema kuwa pamoja na kwamba Real ambayo inastaa mkali Cristiano Ronaldo ilishinda lakini ukweli unabaki kuwa kama wakikutana na Liverpool, ambayo kwa sasa ina nyota ‘kichaa’ Mohamed Salah wajiandae kukumbwa na hali ngumu.
Kikosi cha kocha Zinedine Zidane kinasaka kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo na wameanza vizuri kampeni yao ya nusu fainali kwa ushindi dhidi ya Bayern Munich.
Bellamy alisema kuwa anatamani Bayern Munich ipindue matokeo na kutua fainali ili kuipa upinzani wa kutosha Liverpool.
“Naamini hata mashabiki wa Liverpool wanatamani kukutana na Bayern Munich kwa kuwa wanaamini ushindani utakuwa mkubwa.
Real Madrid imeshapata kikombe mara mbili mfululizo, kwa hiyo ushindani wao unaweza kuwa wa wastani.”
Chanzo: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako