Kumbe mkude kasharejea mazoezini


Na George Mganga 
Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude, ameanza mazoezi mepesi leo ikiwa ni siku moja imesalia kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Njombe Mji FC.
Mkude aliumia wakati Simba ikijifua kwenye Uwanja wa Boko Veterani baada ya kukwaana na Mzamiru Yassin kisha kupelekea kuumia kifundo cha mguu wake.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba SC, inaeleza kuwa Daktari wa timu, Yassin Gembe, amesema hali yake inaendelea vizuri kwa sasa.
"Hali ya Mkude imeendelea kuimarika zaidi na zaidi, leo ameanza mazoezi mepesi na kikosi chetu. Hali yake kwa sasa ni nzuri na ameshaanza mazoezi"  alisema Gembe.
Kikosi cha simba kipo mjini Iringa hivi sasa na kesho kitaanza safari kuelekea Njombe kwa ajili ya mchezo dhidi ya Njombe Mji FC utakaopigwa Sabasaba Stadium Aprili 3 2018.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako