Kocha Mtibwa afunguka ubora wa Dilunga.

Dilunga ajishangilia moja ya goli alilofunga VPL na Captain wake. (Picha na Lebab)
Ni ukweli usiopingika kwamba kwa sasa Hassan Dilunga yupo kwenye kiwango cha juu miongoni mwa wachezaji wa Tanzania wanaocheza eneo la kiungo wa ushambuliaji.
Dilunga ameonesha ubora wake katika mechi kadhaa za hivi karibuni alipoiwakilisha Mtibwa. Mechi ya robo fainali ya ASFC dhidi ya Azam, mchezo wa ligi dhidi ya Singida United pamoja na Simba na nusu fainali ya ASFC dhidi ya Stand United.
Kocha wake Zubery Katwila amesema wakati anamsajili Dilunga alimwambia atamsaidia kuboresha zaidi kiwango chake.
“Tangu anakuja huku (Mtibwa Sugar) nilimwambia kiwango chako kitarudi na kitakuwa juu zaidi kutokana na timu yetu inavyofanya mazoezi naona kwa sasa kiwango chake kinaonekana.”
“Mtibwa wachezaji wanaingia na kutoka, kila mwaka tunachukuliwa wachezaji kwa hiyo tusipowaamini hawa huko mbele wachezaji watakuwa wageni.”
“Tunawapa nafasi zilizoachwa na wachezaji waliotoka ndiyo maana wakati wote timu inaonekana na nguvu na inapambana habadiliki sana kwa sababu nawatumia vijana kuwarithisha sehemu zilizoachwa.”-

posted by Lebab
chanzo: Spoti tz1
MaoniMaoni Yako