Wednesday, April 4, 2018

Kapombe awa mchezaji bora wa simba

Tags

Na George Mganga
Mchezaji wa klabu ya Simba, Shomari Kapombe, ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji FC, uliochezwa leo katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Kapombe ametangazwa baada ya kujipatia kura kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo zilizopigwa kupitia kupitia kurasa za klabu hiyo (Facebook na Instagram), leo.
Beki huyo alisaidia kutengeneza bao la pili alilofunga John Bocco katika mchezo dhidi ya Njombe Mji FC.
Simba ilikuwa na kibarua dhidi ya Njombe Mji FC jioni ya leo na imeweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Bocco. 
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz