Kamati ya watu 12 wa simba kuelekea njombe kuhakikisha ushindi wa simba dhidi ya njombe mji

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Njombe Mji utakaopigwa keshokutwa Jumanne mjini Njombe, Simba wamejipanga kupeleka majina ya watu 12 kutia hamasa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali, amesema leo wanaenda na kamati ya watu 12 walioandaliwa kwa ajili kuongeza nguvu kuhakikisha ushindi unapatikana.
Dalali ameeleza lengo kubwa la kwenda na watu hao 'hajataja majina' ni kuongeza hamasa na morali kwa wachezaji ili kikosi kiweze kupata matokeo.
Simba ipo Iringa hivi sasa ikijiandaa na mechi hiyo kabla ya kuanza safari ya Njombe kesho Jumatatu .
Mchezo huo tutapigwa majira ya saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako