Julio asema "Sioni beki wa Yanga atakaeweza Kuwakaba hawa"

Mchezaji wa zamani wa Simba pia amewahi kuifundisha timu hiyo kwa nyakati tofauti kocha Jamhiri Kihwelu ‘Julio’ anatamani Simba ipate ushindi Yanga siku ya Jumapili Aprili 29, 2018 ili kujihakikishia ubingwa wa ligi msimu huu.


Julio amesema kwa sasa haoni beki wa Yanga ambaye anaweza kuwazuia washambuliaji wa Simba Emanuel Okwi na John Bocco ambao wapo kwenye ubora wao wa kutupia kambani.

“Upande wangu napenda tuwafunge Yanga kwa sababu naamini tukishawafunga tayari tunakuwa mabingwa, lakini kama watatufunga wataanza kutuletea ugumu kwenda kwenye ubingwa.”
“Si dhani kama kuna beki kwa kipindi hiki wa kuweza kumkaba Okwi au John Bocco wengine sitakikuwasema mambo ni mepesi yanaeleweka.”

“Yanga wajipange, tupo vizuri sidhani kama kipindi cha kwanza watamaliza hawajachezea tatu.”


Source: Udaku special

MaoniMaoni Yako