Jose Mourinho asema Anajutia Kauli hizi Alizowahi Kumtamkia Wenger! Hii ni kuelekea Katika Mchezo wa leo Ma United/ Asrenal


Kocha wa Arsenal Arsene Wenger leo siku ya April 29 /2018 ataingia katika uwanja wa Old Trafford kwa mara ya mwisho akiwa kama kocha wa Arsenal kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu, imezoeleka mara nyingi Wenger akikaribia kucheza na timu inayofundishwa na Jose Mourinho huwa kuna kauli za vijembe zinatawala.

Leo April 29 kuelekea mchezo huo Jose Mourinho akiongea na waandishi wa habari ameongea kauli tofauti na kuonesha kusikitishwa kwake na kauli mbaya na kejeli alizowahi kumtolea kocha Arsene Wenger kipindi cha nyuma, Wenger alikuwa na upinzani mkubwa na Man United kipindi inafundishwa na Sir Alex Ferguson lakini mara nyingi yeye na Mourinho wameonekana kuwa upinzani zaidi timu zao zinapokutana.

Jose Mourinho aliwahi kutoa kauli mbalimbali kwa Wenger zinazoonesha kejeli kama ‘mtaalam wa kufeli’ lakini October 2014 waliwahi kuzozana uso kwa uso kiasi cha kusukumana kutokana na kupishana kauli alipoulizwa na waandishi kuhusu hilo Mourinho “Ndio najutia kwa kauli mbovu nilizowahi kutoa kama ambavyo yeye alifanya” Aliongea Jose.


Souerce: Udaku special
MaoniMaoni Yako