Jose Mourinho :Anaamini kwamba haiwezekani kukimbizana na Manchester City msimu huu


Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anaamini kwamba haiwezekani kukimbizana na Manchester City msimu huu huku klabu hiyo ya Etihad ikikaribia kushinda taji la Ligi ya Premia.
City walilaza Everton 3-1 Jumamosi, na hiyo ina maana kwamba watashinda taji kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2013-2014 iwapo watafanikiwa kuwalaza United uwanjani Etihad wikendi ijayo.
United, ambao wanashikilia nafasi ya pili, wana alama 68 baada ya kucheza mechi 31.
Jedwali:Nafasi ya Man Utd
1Man City316784
2Man Utd313768
Lakini wameachwa nyuma na City kwa alama 16.
"Katika ligi nyingine, tungekuwa bado tunapigania taji," amesema Mourinho.
United wamo mbioni kumaliza ligi wakiwa na alama za juu zaidi Ligi ya Premia kwao tangu msimu walioshinda ligi 2012-13 wakiwa na Sir Alex Ferguson msimu wake wa mwisho kwenye usukani.
Misimu iliyofuata, walimaliza nafasi ya saba, nne, tano na sita.Alama zao ni sawa na walizokuwa nazo Tottenham msimu uliopita baada ya kucheza mechi 31.Vijana hao wa Mauricio Pochettino walikuwa wakati huo alama saba pekee nyuma ya viongozi Chelsea.
Lakini baada ya kuondolewa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya hatua ya 16 bora na Sevilla, na kisha kutuhumiwa kwa kucheza mchezo usio wa kuvutia, Mourinho amekosolewa sana msimu wake wa pili akiwa kwenye usukani United.
Source: bbc
MaoniMaoni Yako