Hakuna namna ili pasaka iendelee lazima mmoja afe pale Namfua

Na George Mganga 
Dimba la Namfua litakuwa na kibarua kizito leo ambapo wenyeji Singida United watakuwa wanaikaribisha Yanga katika mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Mchezo huo ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka Tanzania, utafanyika saa 10 kamili jioni ya leo
Timu zote zimeonesha kujitamba huku kila mmoja akisema anahitaji ushindi ili kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Tayari Azam FC, Tanzania Prisons na Njombe Mji wameshaaga hatua ya robo fainali na kushindwa kuiona nusu fainali baada ya kuondoshwa kwa vipigo na wapinzani waliopangiwa nao.
JKT Tanzania, Stand United na Mtibwa Sugar ndizo timu zilizoingia nusu fainali huku zikisubiri kama zinaweza kuungana na Singida United ama Yanga wanaocheza leo.
Hakuna namna, ni lazima mmoja wao apoteze leo ili aondoke na mwingine asonge hatua inayofuata kuingia nne bora ya nusu fainali.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako