Wednesday, April 4, 2018

GOAL OF THE YEAR .

Tags


Ronaldo scores

  • Ronaldo amefunga mabao 19 mechi zake tisa za karibuni zaidi akichezea Real - 25 mechi 13 alizochezea nchi yake na klabu karibuni zaidi
  • Amefunga mabao 39 mechi 36 alizochezea Real msimu huu - mabao mengi kushinda mchezaji mwingine yeyote yule anayecheza ligi tano kuu za Ulaya (England, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uhispania)
  • Amefunga mabao katika mechi 10 alizocheza karibuni zaidi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mtawalia - tisa msimu huu na wakati wa fainali msimu uliopita - kwa jumla amefunga mabao 16
  • Ronaldo ndiye mfungaji mabao bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya akiwa na mabao 119 - mabao 19 mbele ya Lionel Messi wa Barcelona.
  • Amefunga mabao tisa kati ya makombora yake 11 yaliyolenga lango dhidi ya kipa maarufu Gianluigi Buffon.
  • Ronaldo amekuwa akifungia Real Madrid bao la kwanza mechi za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katika mechi 10 kati ya 14 walizocheza karibuni zaidi
  • Amefunga mabao 22 robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, moja zaidi ya Juventus. Ni timu tano pekee, ikiwemo Real Madrid, ambazo zimefunga zaidi ya hapo hatua hiyo.
  • Ronaldo amefunga (14) au kusaidia ufungaji (mara tatu) 68% wa mabao yote 25 ya Real Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu
  • Amefunga katika kila mechi sita alizocheza dhidi ya Juventus - mabao tisa kwa jumla. Hakuna mchezaji aliyefunga mabao zaidi dhidi ya timu moja Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kuliko yeye.