Dismas ten aeleza anayopitia Ngoma

Ofisa Habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten, ameandika machache kuhusiana na mchezaji wa timu hiyo, Mzimbabwe, Donald Ngoma, ambaye hajaonekana Uwanjani kwa muda mrefu. Ten ameamua kuelezea uhalisia wa mchezaji huyo kupitia changamoto za kuwa majeruhi kutokana na kutoonekana kwake Uwanjani kwa takribani msimu mzima wa 2017/18. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Teni ameandika ujumbe akieleza kuwa maisha ni changamoto hivyo kuna wakati lazima uzipitie ili uweze kushinda. "Ndiyo maana yakaitwa maisha, kuna wakati ni lazima upitie changamoto ili kuyashinda" aliandika Ten. Source: Saleh Jembe Na: Agape Patrick Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako