Diamond Platnumz Tena! Atunukiwa Tuzo hii kutoka YoutubeMsanii Pekee Mwenye Subscribers 1,000,000 na zaidi Katika Nchi hizo

Kuna jitihada kubwa sana Youtube hufanya ili kutambua bidii na ushawishi ambao wamiliki wa account za youtube wanao, Moja wapo za jitihana hizi ni kuwatunuku zawadi ya “gold play button” watu waliofikisha subsribers zaidi ya milioni moja kwenye channel zao, Kupata subscribers milioni moja sio shughuli ya lele mama na inahitaji uwe zaidi ya competent ili upewe hii gold play ya youtube


Kuna wengi waliodhani kijana hatoweza na bado wapo watu wengine wasiomtakia mema lakini kijana anaendelea kutia mchanga vitumbua vya hao watu, Kwakweli kijana anatuwakilisha vyema nchi yetu na wengi huwa hatushangai akipendekezwa kuwa rasilimali ya taifa.

Iwe kuchukiwa na wasiompenda, kuitwa majina mabaya, kubanwa na media ama habari za kumchafua huyu dogo hakati tama hadi wengi kumdhania sio mtu wa hii Tanzania, Pindi inapotokea akidhaniwa hawezi kufanya kitu fulani ama akikatazwa kukifanya kwake ni kama unatia mafuta kwenye petroli maana atapambana hadi atekeleze ambayo huwa tunaona hayawezekani kwa wasanii wengi wa Tanzania.

Achilia mbali umaarufu wake ambao nao umechangia kupata hio zawadi ya subscribers milioni 1, Huyu kijana ni mtu anaeweza kuchanganyika na na jamii kwa kutokua na dharau tulizozizoe pindi mtu akiwa star, Kijana kachangamka sana (haboi) na wala hana shobo za kudharau watu kama baadhi ya wapinzani wake.

Yote kwa yote kijana tunampongeza na aendelee kuchapa mzigo na asije kukata tamaa kwajili ya watu ama vitu visvyo na msingi (mfano kelele za teams)

Source:Udaku special
MaoniMaoni Yako