Diamond Platnumz amtakia Ali Kiba heri katika maisha ya ndoa ampa salamu hizi


Licha ya kuwepo na  uvumi kila siku kila uchwao miaka na miaka kuwa diamond platnumz na alikiba wana bifu
Bado wao hupinga suala hilo kwenye media mbalimbali TZ
Huku na kule hapa na pale leo wana wa kariakoo na mwanao alikiba walikua wakifurahia siku ya leo kutokana na king kiba al maarufu kama Alikiba alikuwa anafunga ndoa na mwanadada kutoka kenya anaitwa amina

Shamra shamra zilianza toka asubuhi na bado zinaendelea hadi muda huu na sasa harusi iyo ipo live Azam kupitia channel yao ya Sinema zetu

Twende kwenye mada kuu kwamba diamond amemtakia kila la kheri king kiba katika maisha yake ya ndoa bila kinyongo chochote kwa kupost post hii hapa instagram 👇👇👇👇👇
Hivyo diamond ameendelea kuthibitisha hakuna ugomvi kati yao zaidi ya upinzani wa biashara tuu.

Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

MaoniMaoni Yako