Diamond Na Jason Derulo wafanya kweli Katika Wimbo Wa Kombe la Dunia 2018


Diamond Platnumz, ameendelea kuuthibitishia umma wa ulimwengu kwamba yeye ni Alama ya Taifa katika uwanda wa Muziki kwakuwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuitangaza Nchi ya Tanzania na kuiweka katika Ramani ya Dunia katika Tasnia hii ya Muziki.
Uhodari wa Diamond Platnumz unazidi kuonekana, hivi karibuni alifanya Ngoma matata kabisa inayoenda kwa jina la "African Beauty" aliyomshirikisha Msanii toka Marekani - Omarion. Lakini hilo siyo la mwisho, Diamond alichaguliwa kushiriki kutunga na kuimba wimbo wa kwa ajili ya Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Dunia 2018 yatakayofanyika nchini Rusia.Diamond alipata nafasi hiyo ya kufanya ngoma itakayofungua fainali hizo za kombe la Dunia akishirikiana na Msanii mwingine maarufu kutoka Marekani anaeitwa Jason Derulo. wawili hao tayari wameshatoa Ngoma hiyo itakayotumika katika Mashindano hayo ya Kombe La Dunia Rusia. Hii inamaana kwamba katika matangazo yote ya Kombe la Dunia Yatasindikizwa na Ngoma hii ya Jason na Diamond!

Kwa hakika huu wimbo utakuwa wenye manufaa sana kwa Tanzania, Ni wimbo ambao utatumika kuitangaza Tanzania na utamaduni wake hasa katika kipengele cha Lugha. hii inatokana na ukweli kwamba Diamond, pamoja na kukifahamu Kiingereza kwa uzuri kabisa, ameamua kutumia Ligha ya Kiswahili katika Ubeti aliouimba... kwa hili heko kwako Diamond

Kwaleo hapa, ninakuletea Audio ya ya Wimbo huo nawe mwenzangu uburudike: Tuvipende vya kwetu! Diamond na Jason hawa hapa, wasikilize:
Na: sabby@spoti.co.tz