Diamond na Hamisa wanogesha Tunzo za SZIFF


Ilikuwa ni katika hafla iliyoandaliwa na Azam, iliyohusu utoaji wa Tunzo kwa wasanii mbalimbali wa Tansinia ya Filamu. Ukumbi ulipendeza haswa, ukijumuisha watu mbalimbali wa rika na wadhifa tofautitofauti!

Miongoni mwa watu waliokuwepo katika ukumbi ni msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul almaarufu Diamond Platnumz. Kama haitoshi katika ukumbi pia walikuwepo wasanii kama Wema Sepetu, msanii maarufu wa filamu za kihindi almaarufu kama Aaliyah,alikuwepo pia mnogesha video za nyimbo za bongo fleva bibie Hamisa Mobeto na mchekeshaji Idris Sultan.
Kivutio kikubwa kilikuwa ni uwepo wa Hamisa, Diamond, Wema na Idris.

Ilifika wakati Mshereheshaji wa Shughuli alivomwendea Hamisa na kumuuliza "ulivyokuja hapa ni mwanaume gani ulitamani kama ungemuona na hakika umemuona na unadhani kapendeza na pia uwepo wake kukufurahisha"? Bibie Hamisa bila kumung'unya maneno akajibu "Diamond"
Kamera za ukumbini zilimuonesha Diamond akishangaa na kutikisa kichwa akiwa kajawa na tabasamu  lisiloelezeka. Upande mwingine Wema alionekana kama asiye na furaha kabisa na asiye na habari na kilichokuwa kinaendelea ingawa wenye macho waliona.
Idris naye alivoulizwa swali kama la Hamisa, yeye alijibu kwamba alitamani kumuona Gabo!

Diamond na Hamisa walipata wasaa wa kuwa pamoja na hata Diamond kumshika mkono Hamisa na kumshusha kutoka katika jukwaa kwa upendo mkubwa, wazungu wanasema "gently" Diamond held Hamisa with Compassion!  Hii ilikuwa ni pale Diamond na Hamisa walipotakiwa kukabidhi Tunzo kwa moja ya washindi wa Tunzo hizo. Ukumbi ulilipuka kwa kelele na makofi kitu ambacho kilinogesha shughuli nzima.

Na: Sabinussysevetu@gmail.com
MaoniMaoni Yako