Diamond amfagilia Vanessa Mdee, “Unapambana sana Vee”

Msanii Diamond Platnumz amemfagilia mrembo Vanessa Mdee kutokana na jitihada zake anazofanya kila kukicha za kuupambania muziki wake uzidi kufika mbali zaidi.

Mkali huyo wa WCB kupitia mtandao wake wa Instagram ameandika ujumbe huo wa kumsifia Vee Money huku akimtakia baraka tele kwenye safari yake hiyo.

“Unapambana Sana Vee.. Mwenyez Mungu azidi kukufungulia Kwenye kila la Kheri Uliombalo @vanessamdee 🔥🔥,” ameandika Diamond.

Diamond amewahi kufanya kazi na Vanessa kwa kumshirikisha kwenye ngoma yake inayoitwa ‘Far Away’ ambayo inapatikana kwenye albamu yake ya A Boy From Tandale.
Chanzo: Bongo5
MaoniMaoni Yako