BONDIA ANTHONY JOSHUA AMCHAKAZA PARKER, AFIKISHA MAPAMBANO 21 BILA KUPOTEZA

Hapo tarehe 31/03 usiku bondia Muingereza, Anthony Joshua alifanikiwa kuongeza taji jingine katika mataji matatu aliyokua akishikilia ya WBA, IBO na WBF. Joshua alifanikiwa kuongeza taji la WBO kwa kumpiga bondia kutoka New Zealand, Joseph Parker.

Joshua ambaye alionekana kuongezeka kwa ukali wake na utaalam wa kupiga makonde kwa ujuzi wa hali ya juu alifanikiwa kucheza na kumdhibiti mpinzani wake katika raundi nyingi zaidi za mchezo huo.

Speed ya Parker haikuweza kufua dafu mbele ya mwili wa Anthony Joshau ambao ulionekana kumuelemea Parker kila wakati alipokua akirusha makonde na kutua maungoni mwa Parker.
Ulikua ni mchezo mzuri uliopigwa katika uwanja wa Principality na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali pamoja na zaidi ya mashabiki 80,000 kutazama pambano hilo na wengine sehem mbalimbali walioshuhudia kupitia televisheni.

Joshua alishinda kwa ushindi wa alama 118-112 na 119-111 ambazo majaji wa pambano hilo walizitoa. 

Mbwembwe za Anthony Joshua wakati wa kuingia ulingoni

 Anthony Joshua akionywa na refa baada ya kujaribu kurusha uppercut wakati kengele imelia

 Parker akiinama kukwepa Ngumi jiwe  ya Joshua