Bocco anguruma njombe


Magoli mawili ya mshambulia John Bocco wa Simba yameipa ushindi timu yake dhidi ya Njombe Mji kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara na kufikisha pointi 49 pointi tatu mbele ya Yanga ambayo ipo nafasi ya pili.
Bocco alifunga goli la kwanza dakika ya 17 na dakika ya 64 na kuizima kabisa Njombe Mji ambayo ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 18 kwenye msimamo wa ligi inapambana isishuke daraja.
Baada ya mchezo, Bocco amesema pamoja na wachezaji wengine watapambana kuhakikisha wanapata pointi tatu katika kila mchezo.
“Ushindani bado mkubwa, kuna timu zinapambana kwenda juu na nyingine zinapambana zisiende chini. Mimi na wenzangu tutapambana kwa kila hali na kila uwanja iwe nyumbani au ugenini kuhakikisha tunapata pointi tatu kwa kila mchezo”-John Raphael Bocco mwamuzi wa mchezo wa leo.
Source: Shaffih Dauda
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako