Arjen Robben Afichua kuwa alikaribia kujiunga na Man Utd Mnamo Mwaka 2003.

Arjen Robben amefichua kuwa alikuwa tayari kujiunga na Man Utd baada kula chakula cha usiku na Sir Alex Ferguson mwaka 2003 - lakini hawakumpa ofa yoyote ile ya mkataba.
Star huyo wa uholanzi alisafiri mpaka Carrington kipindi akiwa na miaka 19  desemba 2003 kukutana na Ferguson kueleka uhamisho wake kutoka PSV Eindhoven.
Baada ya kukutana, Robben Alirudi mpaka Eindhoven akiamini alikuwa anatarajia kujiunga na chipukizi mwingine machachari - Cristiano Ronaldo ndani ya Old Traffors ila united Hawakuwa tayar kuafkiana bei iliyotakiwa na PSV juu ya Robben..
Kwahiyo ikaipa nafasi Chelsea mwishowe wakamsajiri kijana huyo kutoka PSV na kuwa na mafanikio na kiwango cha juu sanaa.
Robben ambaye sasa anakipiga katika klabu ya Bayern Munichen Akiwa na Umri wa Miaka 31 Bado yupo katika kiwango kizuri sanaaa..
Posted by Lebabtv
Source: Sky Sports.
MaoniMaoni Yako