Yanga yasisitiza imeshamkamata mwizi wao


Msemaji wa Yanga, Dismas Ten ameendelea kutamba kwamba wana nafasi kubwa ya kuishusha Simba kileleni.
Dismas amesema kama ni kumkimbiza mwizi, tayari wamemshika.
“Ni tofauti ya pointi tatu, lakini sasa ni sawa kwa kuwa wana mchezo ambao haujachezwa na hauwezi kusema ni uhakika.
“Tunaendelea kumkimbiza mwizi kimyakimya, tunasema tumemshika na akituponyoka tutaendelea kimyakimya hadi tumshike,” alisema.
Yanga ipo kambini mjini Morogoro ikijiandaa na mechi yake ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United.
Msemaji huyo amesisitiza kila kitu kinakwenda vizuri na Yanga wanaendelea na maandalizi hayo kwa kuwa Singida wana kikosi kizuri lakini wao, wana kikosi bora zaidi.

Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
Source: saleh jembe
MaoniMaoni Yako