Yanga kupiga tizi la mwisho kesho wachezaji wote wapo fiti

Na George Mganga 
Kikosi cha Yanga kesho kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Namfua kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Singida United.
Yanga ambayo ilikuwa imeweka kambi ya muda mfupi mjini Morogoro, tayari ipo Singida huku ikielezwa wachezaji wake wote wapo fiti kiafya.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema wachezaji wote wapo sawa kuelekea mchezo huo, na jukumu limesalia kwa Mwalimu, George Lwandamina, kuamua nani amuanzishe.
Singida itakuwa inaikaribisha Yanga ikiwa na kumbukumbu za kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye mechi ya ligi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa Namfua Stadium.
Raundi hii zitakutana tena Aprili Mosi 2018 ikiwa ni katika Kombe la FA 
Timu itakayoshinda katika mechi hiyo itaungana na Stand United ya Shinyanga kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho iliyotinga leo kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Njombe Mji FC.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako