Powered by Blogger.

Slider

Breaking

MICHEZO

HABARI

MAGAZETI

UDAKU

BURUDANI

VIDEOS

» » Wizkid Achukua Maamuzi Mazito Baada Ya Kuzinguana Na Drake.Sasa ukweli ni kwamba ingawaje walizinguana na baadaye kuonekana kupatana ukweli ni kwamba kitendo cha Drake kutoonekana kwenye video hiyo bado kilikuwa kinamuumiza sana Wizkid mpaka leo.
Wizkid amesema kuanzia mwaka huu hata’shoot tena video yoyote ile nje ya bara la Afrika na video zote ambazo amesha’shoot nchini Marekani hataziachia.
Akizungumza kwenye mahojiano yake Jumamosi iliyopita na kituo cha Redio cha The Beat 99.9 FM cha nchini Nigeria, Wizkid amesema maamuzi hayo aliyapanga toka mwaka jana baada ya kuona hakuna umuhimu wa kupoteza hela nyingi kwa ajili ya ku’shoot video ughaibuni.
Nimeamua kwa sasa sita’shoot tena video zangu nje ya nchi, Nataka nifanyie video zangu na kila kitu hapa hapa Afrika, Kwa hiyo hata video zangu nilizo’shoot mjini Los Angeles (Marekani) sitazitumia tena,“amesema Wizkid baada ya kuulizwa swali lililohoji kwanini kwenye albamu yake ya ‘Sound From The Other Side’ hakuna hata video moja.
Hata hivyo, taarifa hizo hazijapokelewa vizuri na mashabiki wake huku wengi wakihusisha maamuzi hayo kuwa yamekuja baada Drake mwaka jana kutoonekana kwenye video ya Come Closer.
Na Richard Shiyo richard@spoti.co.tz

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post