Wachezaji wa Yanga Waliokua Kambini ya Taifa Waelekea Morogoro Kuungana na Wenzao


Wachezaji wa Yanga waliokuwa kambini na timu ya taifa, Taifa Stars, leo wanatarajia kusafiri kuelekea mkoani Morogoro kujiunga na kikosi chao kinachojiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Singida United.

Yanga imeweka kambi Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United utakaopigwa Aprili Mosi 2018 kwenye Uwanja wa Namfua, mjini Singida.

Ibrahim Ajib, Hassan Kessy, Kelvin Yondan na Gadiel Michael wataondoka mchana wa leo kwenda Morogoro kuungana na wachezaji wenzao ambao wameweka kambi maalum mjini humo.

Golipika Ramadhan Kabwili, hatoweza kusafiri kutokana na majukumu mengine ya kuitumikia timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, inayojiandaa na mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON U20.

Ngorongoro inajiandaa kucheza mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON U20 dhidi ya DR Congo Machi 31 2018 utakaopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Source:UdakuSpecially
MaoniMaoni Yako