Tshishimbi bana msome hapa kuhusu Ligi Kuu


Kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi raia wa DR Congo, amesema kuwa, wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Singida United pamoja na michuano ya Ligi Kuu Bara.
Yanga na Singida United zinacheza Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Namfua, Singida ambapo mshindi atatinga nusu fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa anapata nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho mwakani.
Wakati Yanga ikiuwaza mchezo huo, pia inapambana kuhakikisha inakuwa bingwa wa Ligi Kuu Bara ambapo kwa sasa ina pointi 46 katika nafasi ya pili, huku Simba ikiongoza ikiwa na pointi kama hizo lakini ikiwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Akizungumzia mchezo huo, Tshishimbi alisema: “Maandalizi yanakwenda vizuri, tutaendelea kupambana katika mechi zetu zijazo kuhakikisha tunafikia malengo.”
“Hakika tunaamini kuwa sasa tupo fiti na tunaweza kuonyesha kiwango chetu kwenye mchezo wowote uliopo mbele yetu.”
Na Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
Chanzo: Championi
MaoniMaoni Yako