TP MAZEMBE WAMFUATA KICHUYA TFF, KICHUYA AMTAJA SAMATTAShiza Kichuya.
JUMANNE iliyopita, Shiza Kichuya akiitumikia Taifa Stars alipiga mpira mwingi na kuwavutia maelfu ya mashabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na wale waliokuwa wakishuhudia kwenye runinga. Kuonyesha kuwa kiwango chake kilikuwa kizuri, kiungo huyo wa Simba ameingia kwenye midomo ya Wacongo kwa kuwa aliwakimbiza katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Stars dhidi ya DR Congo uwanjani hapo.

TP Mazembe ni klabu kubwa ya DR Congo, ndiyo klabu ambayo inatajwa kwa kiwango cha juu kuhusishwa na mchezaji huyo licha ya kuwa hawajatoa tamko rasmi kuhusu kumuwania, lakini kuna kitu ambacho tayari kimefanyika. Siyo Kichuya tu, pia beki wa kati Kelvin Yondani ambaye pia ni mchezaji wa Yanga naye aliwavutia W a c o n g o wa timu ya taifa ambao wanaoju l i k a n a kwa jina la Leopards.


Mara baada ya mchezo huo uliomalizika kwa Stars kupata ushindi wa mabao 2-0, benchi la ufundi la DR Congo
liliwafuata mabosi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuhoji uwezo wa wachezaji hao.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao alisema ni faraja kucheza na timu kubwa kama DR Congo na kuvutiwa na viwango vya wachezaji wa Stars akiwemo mkongwe, Yondani na Kichuya. Kidao alisema, Wacongo hao walihoji beki huyo anaichezea klabu gani kutokana na kuonyesha kiwango kikubwa ikiwemo kutimiza majukumu yake ya kuokoa na kupunguza hatari golini kwao.


“Walishangazwa na uwezo mkubwa wa wachezaji wetu, lakini zaidi ilikuwa ni kwa Yondani wa kuweza kuwazuia w a s h a m b u l i a j i wao wakubwa wanaocheza soka la kulipwa Ulaya. “ Y o n d a n i a l i o n y e s h a uwezo mzuri na kuwazidi uwezo hata walinzi wao ambao w a n a c h e z a katika klabu za Ulaya, maana hiyo Yondani kwa umri wake alionao bado ana nafasi ya kwenda kucheza nje ya nchi.

“Pia walivutiwa na Kichuya kwa jinsi ya umri wake ulivyokuwa na kiwango alichokuwa anakionyesha, hizo ni dalili kuwa wachezaji wetu wanao uwezo wa kupata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa baada ya akina Msuva (Simon), na Samatta (Mbwana),” alisema Kidao.

KICHUYA AFUNGUKA Akizungumzia juu ya uwezo wake kuonekana kukua, Kichuya alisema ni kukubali kujifunza kutoka kwa wenzake wakiwemo Msuva anayecheza Difaa Al Jadida ya Morocco na Samatta anayekipiga KRC Genk ya Urusi. “Nadhani kikubwa ni kukubali kujifunza hasa kutoka kwa wachezaji ambao wamenizidi kwa maana ya kuwa wanacheza nje ya nchi kwa sababu wao wanajifunza vitu vingi na wana uwezo mkubwa wa kuchezea mpira kitu ambacho mimi huenda nikawa nakikosa.

“Sasa iwe mazoezini au kwenye mechi hasa tunapokuwa tunacheza na hizi timu zinazokuwa na wachezaji wakubwa jambo la kwanza huwa namsoma anachotaka kufanya kwa umakini mkubwa kabla ya kufanya ninachotaka kukifanya,” alisema Kichuya. Kabla ya kutua Genk, Samatta alikuwa mchezaji wa Simba kama ilivyo kwa Kichuya kisha akatua Mazembe na baadaye akaelekea Genk.

Na Mwandishi wetu: Richard Mlelwa /barua pepe mlelwa@spoti.co.tz
chanzo;champion


MaoniMaoni Yako