Friday, March 30, 2018

TP Mazembe waanza kumvizia Kichuya

Tags

Taarifa zinaeleza kuwa Uongozi wa klabu ya TP Mazembe inayoshiriki Ligi Kuu nchini Congo umeanza harakati za kumuwania nyota wa Simba, Shiza Kichuya.
Kichuya aliyebatizwa kwa jina la Messi wa Bongo na Afisa Habari wa klabu ya Simba,  Haji Manara, inaelezwa Mazembe wamevutiwa na kiwango cha mchezaji huyo ambaye amekuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho.
Kichuya aling'aa katika mchezo wa mwisho kwa kufunga bao la pili wakati Taifa Stars ilipokutana na timu ya taifa ya Congo katika mchezo ambao Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0. 
Mazembe wamedai kuwa na uhusiano mzuri na Simba tangu wamsajili Mshambuliaji Mbwana Samatta anayekipiga kunako ligi ya Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.
Kichuya atakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na TP Mazembe endapo atasajiliwa, na hii ni baada ya Mbwana Samatta pamoja na Patrick Ochan kusajiliwa na timu hiyo.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz