Singida waiambia yanga ijiandae kufungasha virago

 VIRAGO FA

Uongozi wa klabu ya Singida United umeamua kujichimbia kwa kuweka kambi nje ya mji kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Yanga.
Singida United imeweka kambi Magharibi mwa mji huo ikiwa ni siku kadhaa zimesalia kabla ya pambano hilo kufanyika.
Mkurugenzi wa timu hiyo, Festo Yanga, ametamba kwa kuwaambia Yanga wajiandae kuaga mashindano kwani wamejipanga vilivyo.
"Yanga wajiandae kuaga, tumejipanga vilivyo na tumeamua kuweka kambi Magharibi mwa mji wa Singida ili tujiandae vizuri" alisema Sanga.
Mechi hiyo itapigwa katika Uwanja wa Namfua mjini Singida Aprili Mosi 2018
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
Source: Saleh Jembe
MaoniMaoni Yako