Njombe mji waiachia msaala stand united

Na George Mganga 
Stand United imekuwa timu ya kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC), baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Njombe Mji FC.
Timu hiyo kutoka Shinyanga imejipatia bao hilo katika dakika ya 12 kupitia Bigirimana Blaise aliyefanya dakika zote 90 za mchezo kumalizika kwa bao hilo moja pekee.
Njombe Mji imepoteza mechi hiyo ikiwa ina kibarua kingine Aprili 3 2018 cha Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba SC kitachopigwa mjini Njombe kwenye Dimba la Sabasaba.
Stand wameiachia msala Njombe kwa kuindoa Kombe la Shirikisho na sasa itabidi ijipange kwa ajili ya kukabiliana na Simba iliyo na hasira ya kuukosa ubingwa wa ligi kwa takribani miaka mitano.
Baada ya Stand kuingia hatua ya nusu fainali, timu zingine zilizosalia kwenye robo fainali ni Yanga, Singida United, JKT Tanzania, Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar na Azam FC.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako