NIYONZIMA:Nazidi kuimarika ligi tamu na ubingwa ni wa Simba


BAADA ya kurejea mazoezini siku kadhaa zilizopita, Kiungo wa klabu ya Simba, Haruna Niyonzima, amesema hali yake kwa sasa inaendelea vizuri.
Kwa mujibu wa mahojiano kati yake na Radio One kupitia kipindi cha michezo jioni hii, Niyonzima ameeleza kuwa anashukuru Mungu kuona hali yake inaimarika, na akisema anaweza akarejea kikosini hivi karibuni kuanza kucheza.
Aidha, Niyonzima ametamba kwa kusema ligi ni ngumu lakini ni tamu, vilevile amesema ana uhakika ubingwa utatua Msimbazi msimu huu kutokana na namna wanavyoupambania.
Niyonzima amesisitiza kuwa Simba lazima itwae ubinwa wa Ligi Kuu Bara kwani wanataka kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Kiungo huyo amekosekana dimbani kwa muda mrefu kufuatia maumivu ya enka aliyoyapata katika hatua ya mzunguko wa kwanza wa ligi
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
Source: saleh jembe
MaoniMaoni Yako