Niyonzima, Mbonde wampa raha kocha SimbaWCHEZAJI Mnyarwanda Haruna Niyonzima na Salim Mbonde wamerudisha matumaini kwa kocha mkuu wa kikosi hicho, Mrafansa Pierre Lechantre akisema mambo yatakuwa mazuri.


Wachezaji hao Niyonzima ni kiungo na Mbonde ni beki wa kati walikuwa majeruhi wa muda mrefu lakini sasa wamerudi uwanjani na kujiunga na timu ingawa bado wanaendelea na mazoezi ya 'fitinesi' ya kukimbia uwanjani na baadaye ndiyo watajiunga na wenzao kwa ajili ya ufundi.


"Kwetu ni jambo zuri kwa sababu tunakuwa na upana wa wachezaji na hata katika mechi zetu itakuwa rahisi, bado wanaendelea na mazoezi mepesi nafikiri siku mbili tatu tutakuwa nao,"alisema Lechantre.


Ameongeza na kusema, kuwa na upana mkubwa wa wachezaji ni nzuri kwa timu kwa sababu inaongeza ushindani.


Simba inaendelea na mazoezi yake Uanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Njombe Mji ya Njombe. 
Na Mwandishi wetu: Richard Mlelwa /barua pepe mlelwa@spoti.co.tz
Chanzo: Mwanaspoti