Ngoma na Kamusoko fiti kuwavaa singida utd kesho

Na George Mganga 
Baada ya kuwasilini mjini Singida salama jana, kikosi cha Yanga kinafanya mazoezi ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Namfua.

Yanga iliwasili mjini humo ikiwa ina kibarua cha mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United utakaopigwa siku ya Pasaka Aprili Mosi 2018.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, jana alisema wachezaji wote wapo fiti kuanza na jukumu litabakia kwa Kocha George Lwandamina kuamua yupi amtumie.

Mchezo huo unataraji kuanza majira ya saa 10 kamili jioni ambapo mshindi ataungana na timu zitakazokuwa zimetinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Stand United ndiyo timu ya kwanza kuingia hatua ya nusu fainali kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Njombe Mji jana, mechi iliyopigwa Kambarage Stadium.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako