Neema inarudi jangwani Ngoma mambo safi tu kambini Moro
Wakati Yanga ikiwa katika maandalizi kuelekea mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Singida United mjini Singida, inaelezwa hali ya Donald Ngoma inazidi kuimarika.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh, amesema mchezaji huyo ameanza kuimarika taratibu pia ameshiriki mazoezi ya siku mbili na wenzake.
Ngoma amekuwa akifanya mazoezi yote ambayo yanatolewa na Kocha wa timu hiyo asubuhi na jioni.
Mshambuliaji huyo aliumia Septemba 30 2017 katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Yanga imeweka kambi ya muda mfupi mjini Morogoro kabla ya kuelekea Singida ambapo Aprili Mosi itakuwa ina kibarua cha mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United.
Email: agape@spoti.co.tz
Source:SalehJembe