Mwamuzi wa Kenya Kusimamia Mechi Kombe la Dunia 2018


Aden Marwa ni miongoni mwa waamuzi wasaidizi 10 kutoka Afrika watakaosimamia mechi za kombe la dunia.
Mwamuzi huyo mwenye uzoefu wa miaka 7 akifanya kazi na shirika la FIFA,alifanikiwa kuorodheshwa kwenye orodha ya mwisho kwa ajili ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Hata hivyo hakufanikiwa kusimamia mechi yeyote.
FIFA imechagua maafisa 6 kutoka barani Afrika kusimamia mechi za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Urusi.
Pamoja na hao waamuzi wasaidizi 10 wametoka barani Afrika, kwa ujumla maafisa 99 wamechaguliawa kusimamia michuano hiyo.
Aden Marwa ana uzoefu wa kuwa mwamuzi msaidizi katika michuano ya kombe la dunia la vilabu 2016 nchini Japan.
Alitajwa kuwa mwamuzi msaidizi wa CAF katika shirikisho la kombe la FIFA 2017 na alishiriki pia mwaka 2012,2013, na 2015 kwenye kombe la mataifa ya Afrika pamoja , kombe la dunia la walio chini ya miaka 17 , michuano ya CAF ya chini ya miaka 23 na kombe la dunia la vilabu la FIFA
Aden Marwa ni nani?
  • Ana umri wa miaka 41
  • Ana uzoefu wa miaka saba akifanya kazi na FIFA
  • Ni Mwalimu wa Sekondari anafundisha masomo ya kemia na hesabu
  • Ametokea kaunti ya Migori, iliyo katikati ya Kenya
Maafisa waliochaguliwa kutoka nchi 46 watashiriki katika semina ya wiki mbili ya chama cha mpira cha Italia kwenye mji wa Coverciano mwezi ujao
Hongera kwa wana wa Africa Mashariki.
Source: BBC Swahili
MaoniMaoni Yako